Kwani Floyd Mayweather kafilisika?
kaamua kuususa mkanda wake? au ndio mwendelezo wa zile mbwembwe zake? Kweli kaamua kuuachia mkanda wake hivihivi kisa deni la Mil 446?
kaamua kuususa mkanda wake? au ndio mwendelezo wa zile mbwembwe zake? Kweli kaamua kuuachia mkanda wake hivihivi kisa deni la Mil 446?
Story ya mwishomwisho kusikika kuhusu yeye ilihusu Shirikisho la Ngumi Duniani WBO kutangaza kumvua mkanda alioshinda baada ya kumpiga Manny Pacquiao kutokana na deni la Dola 200,000 (ni kama Tshs. 446) ambazo ilitakiwa alipie kama kodi baada ya pambano lake na Manny Pacquiao!!
Tukiachana na stori hizo najua kuna mastory mengi kuhusu jamaa kustaafu, maswali kuhusu nani atapanda nae jukwaani hivi karibuni.. ninayo hii list ya Mabondia ambao wametajwa kwamba huenda mmoja wao akapanda kuzipiga nae kabla hajastaafu.
Kiukweli kwenye hii list hakuna mwenye rekodi mbaya, kila mmoja ni mkali yani.
Kell Brook, Jamaa na yeye ana rekodi kali kabisa Ulingoni. Ameshinda mapambano 35, kati ya hayo 24 ni knockout.
Amir Khan, rekodi yake inaonesha kashinda jumla ya Mapambano 31, Mapambano matatu kapigwa na mengine 19 ameshinda kwa knockout.
Karim Mayfield, rekodi yake nae inaonesha ameshinda Mapambano 19, kashindwa Mapambano mawili na Mapambano 11 ameshinda kwa knockout.
Timothy Bradley Jr. Jamaa yuko vizuri aisee, ana ushindi wa Mapambano 31, kapigwa pambano moja na jingine moja ni droo.
Andre Berto. Kwenye list ya Mabondia ambao wako tayari kupambana na jamaa wakati wowote ule, huyu ana rekodi ya kushinda Mapambano 30, kapigwa kwenye Mapambano matatu na mengine 23 ameshinda kwa knockout.
Anaitwa Shawn Porter, ana ushindi wa Mapambano 26 amepigwa pambano moja tu, katoa droo moja na kushinda knockouts 16.
Wakati utafika na tutajua tu nani atakutana ulingoni na mbabe huyu wa karne, swali ni kwamba atakubali rekodi yake ya ushindi wa mapambano 48 iharibike?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni