Kwa kipindi cha kama miezi miwili
katikati ya March na May 2015 hali haikuwa nzuri Afrika Kusini, Xenophobia ilikuwa janga jingine kubwa lililoathiri wageni wengi ndani ya nchi hiyo.
Kulikuwa na machafuko, mitandaoni zikasambaa picha na video zinazoonesha wageni walioko kwenye baadhi ya maeneo ndani ya nchi hiyo wakivamiwa, walikuwepo waliojeruhiwa.
Wengine waliuawa, wapo waliokimbilia kuomba hifadhi japo wawe kwenye mikono salama ya Kambi mbalimbali za Wakimbizi.. lakini wengine waliona South Africa sio mahali salama kwa ajili yao, walirudi kwenye nchi zao.
Baada ya ripoti zote na hali ya hewa kukaa sawa, leo nina stori kuhusu watu waliokamatwa wakihusishwa na kufanya vurugu hizo.. Waziri wa Polisi South Africa, Nathi Nhleko kaitoa ripoti kwenye Kikao cha Bunge la nchi hiyo kwamba idadi ya watu waliokamatwa kwa kufanya vurugu na kushiriki kwenye machafuko hayo wako 9,098.
Waziri huyo anasema bado Oparesheni inaendelea, wanaendelea kuwakamata wahusika wote ila hakutoa ufafanuzi wowote kuhusu hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa watuhumiwa wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni